Maukibu Husseiniyya 450 zinatoa huduma kwa mazuwaru katika wilaya ya Qarnah.

Mawakibu Husseiniyya katika wilaya ya Qarnah mkoani Basra zinatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wanaokwenda Karbala kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Muandishi wetu wa Habari aliye katika wilaya hiyo amesema “Idadi ya mawakibu Husseiniyya zinazohudumia mazuwaru wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) katika wilaya ya Qarnah na zilizo sajiliwa rasmi na kamati ya mawakibu Husseiniyya ya wilaya ni 450 zimejipanga pembezoni mwa Barabara zinazotumiwa na mazuwaru hao”.

Akaongeza kuwa “Mawakibu zinatoa huduma tofauti kama vile chakula, vinywaji, malazi, afya na zinginezo, huduma hizi zitadumu kwa muda wa siku saba takriban, kuanzia mwezi ishirini na tisa Muharam hadi mwezi sita Safar”.

Wilaya ya Qarnah ipo umbali wa (kilometa 441) kutoka Karbala, baada ya misafanya ya mazuwaru kuisha, wahudumu wa mawakibu hizo huanza safari ya kwenda Karbala kufanya ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: