Makamo rais wa kitengo hicho Shekhe Zainul-Aabidina Quraish amesema “Kitengo kimekamilisha maandalizi ya ziara ya Arubaini kwa kuweka vizuwizi vya mbao kwa ajili ya kuongoza matembezi ya mazuwaru pamoja na kutandika kapeti lekundu kwenye maeneo ya kuingia na kutoka mawakibu Husseiniyya”.
Akaongeza kuwa “Vizuwizi vya mbao huwekwa karibu na milango ya Sardabu za Atabatu Abbasiyya kwenye ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, kwa lengo la kuongoza matembezi ya mazuwaru”.
Akabainisha kuwa “Tumeweka utaratibu mzuri wa kuongoza mazuwaru kwa kushirikiana na vitengo vingine, mazuwaru wataingia kwa mistari na kwa vikundi kwa namna ambayo hakutokuwa na msongamano”.
Akaendelea kusema “Watumishi wa kitengo chetu wanaendelea kutimiza wajibu wao, ikiwa ni mapoja na kupuliza marashi ndani ya haram tukufu sambamba na kuandaa mahitaji yote muhimu kwa ajili ya kufanya ibada ya ziara”.