Mazuwaru wanaokwenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) wanaendelea kutembea katika mkoa wa Basra.
Wamefika kaskazini ya mkoa wa Basra, kutokea kitongoji cha Qarnah, wanatarajiwa kutembea umbali wa (km 400) takriban hadi kufika Karbala.
Mawakibu zilizopo barabarani zinatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru, aidha wakazi wamefungua milango ya nyumba zao na kuhudumia mazuwaru.
Mji wa Basra upo kusini mwa Iraq, mazuwaru huanza kutembea katika mji huo kuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ambapo watu wa mikoa mingine ya kusini huungana nao kwenye matembezi hayo.