Chuo kikuu cha Alkafeel kimetoa wito kwa wanafunzi wake washiriki kwenye shughuli za uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza.

Kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel kimetoa wito kwa wanafunzi wake washiriki shughuli za uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza kwa kushirikiana na jumuiya ya mwezi mwekundu ya Iraq tawi la Najafu.

Warsha ya kutoa muongozo na maelekezo inafanywa saa mbili asubuhi hadi saa nane Adhuhuri siku ya Alkhamisi sawa na tarehe (24/8/2023), wanafunzi hao watatoa huduma za afya kwenye maukibu ya chuo kwa mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Mkuu wa kitengo cha udaktari Dokta Samir Maki na wasaidizi wake, wamekutana na ujumbe kutoka jumuiya ya mwezi mwekundu ya Iraq tawi la Najafu na kujadili mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya utoaji wa huduma za afya kwa mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) kupitia maukibu ya chuo kikuu cha Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: