Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha mkarimu wa Ahlulbait Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala, imehudhuriwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru watukufu.

Muhadhiri wa Majlisi hiyo Shekhe Muhammad Kuraitwi amesema “Tumeongea kuhusu historia ya Imamu Hassan (a.s) na mazingira aliyoishi na jinsi alivyojitolea”.

Akaongeza kuwa “Pamoja na changamoto nyingi alizokuwanazo Imamu Hassan (a.s) lakini alitekeleza wajibu wake kwa ufasaha, aliweka misingi ya harakati ya Imamu Hussein (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya harakati mbalimbali za kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) hususan kumbukumbu za vifo, kwa kufanya Majlisi za kuomboleza na kuangazia historia zao takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: