Kitengo cha maelekezo ya kidini katika Atabatu Abbasiyya kimefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha bwana wa vijana wa peponi Imamu Hassan Zakii (a.s).
Kiongozi wa idara ya mahusiano na matukio ya kidini bibi Rajaa Ali, amesema kuwa Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu na Ziaratu-Ashura, ukafuata muhadhara wa kidini kuhusu Imamu Hassan (a.s).
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na qaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za majonzi na huzuni kutokana na dhulma alizofanyiwa Imamu Hassan (a.s).