Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake inaendelea na program ya kuwajengea uwezo wahudumu wa kujitolea katika ziara ya Arubaini.

Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na program ya kuwajengea uwezo wahudumu wa kujitolea katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein.

Kiongozi wa idara bibi Adhraa Shami amesema “Watumishi wa idara wanaendelea kutoa maelekezo kwa wahudumu wa kujitolea kwenye ziara ya Arubaini katika Sardabu ya Alqami ndani ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Program inahusisha muhadhara wenye anuani isemayo (Ukamilifu katika uislamu) uliojikita katika kueleza kutambua njia sahihi ya kufikia malengo ya mwanaadamu, nayo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akaendelea kusema “Program hii inafanywa kwa kushirikiana na idara zingine za wanawake ambazo zinashiriki kikamilifu kumuandaa muhudumu wa kujitolea na kumfanya kuwa msaada mkubwa katika kuhudumia mazuwaru watukufu”.

Mmoja wa wahudumu wa kujitolea bibi Nabaa Mussawi ameshukuru idara ya maelekezo ya kidini kwa kazi kubwa inayofanya ya kuwajengea uwezo wahudumu wa kujitolea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: