Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Haidari Mussawi amesema “Watumishi wa kitengo wamekamilisha maandalizi yote ya ziara ya Arubaini, na kuweka ulinzi kwenye njia zote zinazoelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kimeanza kazi ya kukagua mabegi na mizigo ya mazuwaru kwenye vituo vikuu, mwanzoni mwa njia zinazoelekea Atabatu Abbasiyya, kwa kutumia vifaa vinavyotambua vilipuzi, sambamba na kuzingatia urahisishaji wa matembezi ya mawakibu, gari za wagonjwa na gari zingine za kutoa huduma mbalimbali”.
Akaendelea kusema “watumishi wetu watarahisisha matembezi ya mawakibu Husseiniyya wakati wa kuingia na kutoka ndani ya haram tukufu”, akasema kuwa “Watumishi wa kitengo hiki walipewa semina za utoaji wa huduma ya kwanza na uokozi kwa ajili ya kupambana na hali yeyote inayoweza kutokea wakati wa ziara”.