Majmaa-Ilmi imewapa zawadi wanafunzi wake waliohifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Qur’ani tawi la Najafu, imewapa zawadi wanafunzi wake waliohifadhi juzuu kadhaa za Qur’ani tukufu.

Kiongozi wa idara ya Tahfiidh na maelekezo ya Qur’ani Sayyid Zaidi Maduhi amesema kuwa “Maahadi imewapa zawadi ya pesa wanafunzi waliohifadhi juzuu kadhaa za Qur’ani”.

Akabainisha kuwa “Wamepewa kiashi cha dinari elfu (30) kwa kuhifadhi juzuu moja, kila mwanafunzi amepewa kiwango hicho kwa kila juzuu alilo hifadhi”.

Akaongeza kuwa “Jumla ya wanafunzi (31) wamepata zawadi, wanafunzi wanne wamehifadhi juzuu saba, wanafunzi wawili juzuu sita, wanafunzi nane juzuu tano, wanafunzi wanne juzuu nne, wanafunzi saba juzuu tano na waliobaki baina ya juzuu moja hadi tatu”.

Majmaa-Ilmi kupitia matawi yake yaliyoenea mikoa yote ya Iraq, inafanya kazi kubwa ya kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii, sambamba na kulinda misingi ya uislamu halisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: