Maandalizi ya ziara ya Arubaini.. chuo kikuu cha Alkafeel kimeandaa semina ya utoaji wa huduma ya kwanza na uokozi.

Chuo kikuu cha Alkafeel kimeandaa semina ya utoaji wa huduma ya kwanza na uokozi kwa kushirikiana na jumuiya ya mwezi mwekundu tawi la Najafu kwa wanafunzi wa chuo cha udaktari ili kujiandaa na ziara ya Arubaini.

Semina hiyo imejikita katika kuwatambulisha wanafunzi umuhimu wa utoaji wa huduma ya kwanza na uokozi na jinsi huduma hiyo inavyochangia kwa kiwango kikubwa kuokoa maisha ya watu, semina hiyo ni maalum kwa ajili ya kuhudumia watu wanaokuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Semina imesaidia kujenga uwezo wa uokozi kwa wanafunzi wa udaktari.

Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa huduma bora za afya kwenye vituo vya afya vilivyopo katika mawakibu tatu za chuo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: