Mkufunzi wa kimataifa Dokta Naji Ali Al-Asili ametoa maelekezo ya kiafya kwa mazuwaru wanaokwenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini katika mazingira ya joto kali.
Yafutayo ni maelekezo yaliyotolewa:
- - Kuzingatia kupoza muili kwa kuweka kitambaa kilicholowana maji kichwani, au kutumia mwamvuli wakati unapotembea juani.
- - Kujiepusha kupigwa na jua moja kwa moja kwenye muili wako hususan wakati wa mchana.
- - Kuvaa nguo za koton ambazo husaidia kunyonya jasho linalotoka mwilini.
- - Kunywa vimiminika kwa wingi, hususan maji safi ya kunywa.
Hospitali ya rufaa Alkafeel imetoa maelekezo hayo wakati huu ambao watu wengi wanamiminika katika mji wa Karbala kuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).