Majmaa-Ilmi imefanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wake katika mkoa wa Baabil.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wake katika mkoa wa Baabil.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil Sayyid Muntadhar Mashaikhi amesema “Semina imewalenga watumishi wa Maahadi katika mji wa Baabil, nayo ni sehemu ya harakati ya mradi wa begi la Qur’ani, unaosimamiwa na tawi hilo”.

Akaongeza kuwa “Wanasemina wamefundishwa masomo ya maarifa ya Qur’ani na Fiqhi, sambamba na masomo mengine ya kujenga uwezo wao, chini ya wakufunzi mahiri”.

Akaendelea kusema “Semina imedumu kwa muda wa saa Hamsini, ndani ya kipindi cha miezi miwili, nayo ni sehemu ya mkakati wa Majmaa-Ilmi unaolenga kuwajengea uwezo watumishi wake” akaongeza kuwa “Maahadi itafanya semina zingine za kuwajengea uwezo wakufunzi wa semina za Maahadi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: