(Tauhidi katika Qur’ani) kitabu kipya kimetolewa na kitengo cha Habari na utamaduni.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandika kitabu cha (Tauhidi katika Qur’ani).

Waliosimamia uandishi wa kitabu hicho ni kituo cha kiislamu na tafiti za kimkakati chini ya kitengo.

Kitabu hicho ni sehemu ya mfululizo wa masomo ya Aqida, kimeandikwa na Shekhe Abdullahi Aamili na kutafsiriwa na Shekhe Muhammad Hussein Khaliiq.

Muandishi ameeleza zaidi mada ya Tauhidi ambayo ndio msingi wa uhai wa Imani, hakika mada hiyo ndio mama wa mada zote za Aqida na ndio msingi wa Dini kinadhariyya na kivitendo.

Kitabu kimeanza kwa kumtambulisha Mwenyezi Mungu mtukufu, kisha Utume, Uimamu na kumalizia katika Miaad na kueleza matendo mema na maovu yanayofanywa na mwanaadamu hapa Duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: