Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefungua vituo viwili vya kitamaduni kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein katika mkoa wa Dhiqaar.
Vituo hivyo vinasimamiwa na kamati iliyochini ya kitengo.
Kiongozi wa kituo Shekhe Harithi Dahi amesema “Vituo vimeanza kutoa huduma za kitamaduni kwa mazuwaru wanaoelekea katika mji mtukufu wa Karbala kuhuisha Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Tumefanya warsha iliyohusisha watu wote muhimu katika jamii, iliyofundisha mambo ya kidini, kijamii na kimalezi”.
Akabainisha kuwa “Vituo vinalenga watu wote katika jamii hususan kundi la mijana, kinawafundisha mambo yote ya kitamaduni na kielmimu, ikiwa ni sehemu ya kumtumikia Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.