Njia ya kuelekea peponi.. mkoa wa Muthanna unaaga misafara ya mazuwaru wa Arubaini.

Mazuwaru wanaotembea kwa miguu Kwenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) wamefika wilaya ya mwisho ya mkoa wa Muthanna.

Kwa mujibu wa ribota wetu amesema “Mazuwaru wamefika kwenye wilaya ya Ramitha, kituo cha mwisho cha mkoa, wametembea umbali wa (km 430) kuanzia sehemu ya kwanza ya matembezi yao katika kitongoji cha Raasu-Bishah, bado watatembea umbali wa (km 220) hadi wafike katika mji wa Karbala”.

Akasema kuwa “Mawakibu Husseiniyya zilizojipanga pembeni ya barabara zinatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru hao, huku wakazi wa maeneo wanayopita wakiwa wamefungua milango ya nyumba zao na kujitolea kila wawezalo katika kuhudumia mazuwaru”.

Akaongeza kuwa “Mji wa Ramitha ni wilaya ya mwisho ya mkoa wa Muthanna, baada ya hapo mazuwaru wataingia wilaya ya Hamza, ambayo ni wilaya ya kwanza katika mkoa wa Diwaniyya”.

Mkoa wa Muthanna ni mkoa wa tatu kuingiwa na mazuwaru wanaotoka Basra kusini mwa Iraq, ambapo wakazi wa mikoa ya kati hujiunga nao katika kufanya matembezi ya kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: