Chuo kikuu cha Alkafeel kimefungua mawakibu tatu kwenye Barabara zinazotumiwa na mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kwa ajili ya kutoa huduma za afya.
Rais wa chuo Dokta Nuris Muhammad Dahani amesema “Watumishi wa chuo wanafanya kila wawezalo katika kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) kupitia mawakibu zilizofunguliwa kwenye Barabara zinazotumiwa na mazuwaru wanaotembea kwa miguu”.
Akaongeza kuwa “Mawakibu hizo zinatoa huduma za afya kwa mazuwaru, ikiwa ni pamoja na kujibu maswali ya mazuwaru watukufu sambamba na kuandaa sehemu za kupumzika na ugawaji wa chakula milo mitatu kwa siku”.
Akaendelea kusema “Mawakibu hizo zipo sehemu tatu, sehemu ya kwanza katika mji wa Kufa karibu na malalo ya swahaba mtukufu Maitham Tamari (r.a), sehemu ya pili katika mji wa Najafu karibu na nguzo ya (23) na sehemu ya tatu kwenye Barabara ya Abbasi (a.s) katika mji mtukufu wa Karbala”,