Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi Husseiniyya pembezoni mwa maukibu ya kiongozi wa wasomaji chini ya ushiriki wa jopo la waimbaji na usimamizi wa kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya kitengo.
Majlisi zinafanywa kuanzia usiku wa (11 – 20) katika mwezi wa Safar kwenye Barabara ya Karbala na Najafu karibu na chuo kikuu cha Al-Ameed katika nguzo namba (1238), wanashiriki kwenye Majlisi hizo waimbaji wa Husseiniyya wafuatao (Murtadha Harbi, Ammaar Kinani, Qahtwani Budairi, Muhammad Baaqir Khaqaani, Muhammad Janami, Hassan Swalihi, Murtadha Hamidawi na Ali Saaidi).
Maukibu ya kiongozi wa wasomaji inashughuli mbalimbali, miongoni mwa shughuli zake ni kufundisha Qur’ani na kufanya Majlisi za Husseiniyya.