Hema la bwana wa maji linatoa mihadhara kwa mazuwaru wa Arubaini.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inatoa mihadhara mbalimbali na kusoma Qur’ani kwa mazuwaru wa Arubaini kupitia hema la (bwana wa maji).

Makamo wa kitengo cha taaluma amemuambia rais wa Majmaa Dokta Liwaau Atwiyya kuwa “Hema hili ni sehemu ya harakati za Majmaa-Ilmi ya Qur’ani katika kipindi cha ziara ya Arubaini ya mwaka huu 1445h, limejengwa kwa mara ya kwanza na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Dhiqaar makao makuu ya mkoa wa Naswiriyya sambamba na kuanzisha Maahadi hapa mkoani”.

Akaongeza kuwa hema limetoa huduma tofauti kwa mazuwari wakati wa matembezi yao hapa mkoani.

Mkuu wa Maahadi katika mji wa Dhiqaar Sayyid Ali Bayati amesema “Idara ya harakati imeandaa ratiba inayoendana na mazingira ya ziara, miongoni mwa vipengele vya ratiba hiyo ni usomaji wa Qur’ani na ushiriki wa kikundi cha qaswida za kidini kiitwacho (kijana mwenye nuru)”.

Akaongeza kuwa “Maahadi imeandaa mihadhara kadhaa inayowasilishwa kwa mazuwaru kupitia hema la bwana wa maji, chini ya wahadhiri mahiri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: