Kituo cha ufundi kinaandaa milango ya haram tukufu kwa ajili ya kupokea mazuwaru wa Arubaini.

Kituo cha ufundi katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha kazi ya kuandaa milango ya haram tukufu kwa ajili ya kupokea mazuwaru wa Arubaini na mawakibu Husseiniyya.

Makamo wa kiongozi wa kituo cha ufundi Mhandisi Ammaar Swalahu Mahadi amesema “Watumishi wa kituo wamekamilisha kuandaa mlango wa Kibla na Imamu Hassan (a.s) katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kuweka njia maalum zinazotenganishwa na vizuwizi vya mbao kwa ajili ya kurahisisha misafara ya kuingia na kutoka kwa mazuwaru na mawakibu Husseiniyya”.

Akaongeza kuwa “Kazi hiyo imehusisha milango ya Swahibu Zamaan (a.f) na Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika kuratibu uingiaji wa mazuwaru sambamba na kufunika ngazi ya umeme inayoingia kwenye sardabu ya Imamu Hussein (a.s)”.

Vitengo, idara na vituo vyote vya Atabatu Abbasiyya vinafanya kila aina ya juhudi kuhakikisha vinatoa huduma bora kwa mazuwaru wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wanaokuja kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: