Watumishi wa maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kutekeleza ratiba ya ziara ya Arubaini.
Kiongozi wa idara ya maktaba bibi Nuru Muhammad Ali amesema “Watumishi wa maktaba wameanza kutekeleza ratiba maalum ya ziara ya Arubaini, kupitia maukibu ya Ummul-Banina (a.s) iliyopo katika chuo kikuu cha Al-Ameed, inahusisha mambo ya kitafiti na kielimu kwa lengo la kuongeza uwelewa kwa mazuwaru”.
Akaongeza kuwa “Ratiba hiyo inahusisha maonyesho ya vitabu, mashindano ya aina tofauti kwa wanawake na watoto, sambamba na kuendesha mashindano mengine kupitia mitandao ya kijamii”.
Akaendelea kusema “Maonyesho ya vitabu yamehusisha machapisho ya kitengo cha Habari na utamaduni na majarida yanayo tolewa na Atabatu Abbasiyya, kama jarida la Riyadhu-Zaharaa (a.s) linalochapishwa na Maktaba”.
Akaongeza kuwa “Ratiba hiyo itadumu kwa siku zote za ziara, kwa ajili ya kunufaika na mamilioni ya watu wanaokuja”.