Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani kupitia mradi wa usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru.
Mahafali imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Muthanna chini ya Majmaa.
Mahafali imepambwa na sauti za wasomaji wafuatao (Ali Hussein, Hussein Haitham, Walidi Khalidi na Amiri Ali), wamesoma Qur’ani tukufu katika mazingira yaliyojaa Imani Jirani na mazuwaru wanaotembea kwa miguu Kwenda kwa bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s) katika ziara ya Arubaini.
Mahafali inalenga kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii ya mazuwaru.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu imefungua vituo (52) vya usomaji wa Qur’ani katika mikoa ya (Muthanna, Diwaniyya, Baabil, Baghdad na Karbala takatifu).