Vituo vya Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya vimeshuhudia mwitikio mkubwa wa mazuwaru wa Arubaini wanaokwenda Karbala.
Vituo hivyo vinasimamiwa na maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu ni sehemu ya mradi wa Qur’ani katika ziara ya Arubaini, vinalenga kusahihisha usomaji wa surat Fat-ha, sura fupi fupi, nyeradi za swala, namna ya kutawadha pamoja na kujibu maswali kisheria kutoka kwa mazuwaru wanaokwenda Karbala kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maahadi ya Qur’ani imefungua vituo (7) kwenye Barabara zinazotumiwa na mazuwaru katika maeneo (6) ambayo ni wilaya ya Kufa, Mashkhabu, Munadharah, mtaa wa Radhawiyya, Huriyya, Mahnawiyya na kwenye Barabara ya (Yaa Hussein) baina ya Najafu na Karbala katika maukibu ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kwenye nguzo namba (208).