Njia ya kuelekea peponi.. Baabil inapokea mazuwaru wa Arubaini na wakazi wake wamiminika kupata utukufu wa kuwahudumia.

Miguu ya mazuwaru wanaokwenda Karbala kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) imekanyaga ardhi ya mkoa wa Baabil.

Ripota wetu amesema kuwa “Mazuwaru wamewasili katika kata ya Jarbuiyya mwanzoni mwa wilaya ya Qassim katika mkoa wa Baabil, wametembea umbali wa (km 560) kutoka sehemu yalipoanzia matembezi hayo kwenye kitongoji cha Raasu-Bisha, watatembea umbali wa (km 80) hadi wafike Karbala tukufu”.

Akabainisha kuwa “Baabil inapokea mazuwaru kupitia Barabara zenye bustani nyingi ambazo zinapunguza ukali wa jua kwa mazuwaru, sehemu hizo zimejaa mawakibu zinazohudumia mazuwaru”.

Akaendelea kuwa “Wakazi wamefungua myumba zao na kutoa huduma kwa mazuwaru, huku mawakibu Husseiniyya zikiendelea kuhudumia mazuwaru kila sehemu kwa huduma tofauti hadi sehemu za kupumzika”.

Mkoa wa Baabil ni mkoa wa tano kuingiwa na mazuwaru wanaotoka Basra kusini mwa Iraq, wanaokuja kushiriki kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: