mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria anaangalia huduma zinazotolewa na maukibu ya Ummul-Banina (a.s) katika chuo kikuu cha Al-Ameed.

Kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami, ameangalia huduma zinazotolewa na maukibu ya Ummul-Banina (a.s) katika chuo kikuu cha Al-Ameed kwa mazuwaru wa Arubaini.

Katika ziara yake amekutana na msimamizi mkuu wa maukibu Sayyid Majidi Muhammad, ambaye amemuonyesha huduma mbalimbali zinazotolewa kwa mazuwaru wanaoelekea Karbala kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Shami akasisitiza kuongeza juhudi katika utoaji wa huduma kwa mazuwaru na kufanya kazi muda wote kulingana na mahitaji yanayotokana na kuendelea kuongezeka kwa idadi ya mazuwaru.

Maukibu ya Ummul-Banina imekuwa ikitoa huduma tofauti kwa mazuwaru kwa siku kadhaa sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: