Mkoa wa Wausitu.. mawakibu elfu tatu zinatoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini.

Zaidi ya maukibu elfu tatu zimeshiriki kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Waasit.

Muwakilishi wa mawakibu hizo hapo mkoani Sayyid Ali Rahim Atabi amesema “Kama kawaida ya watu wa Waasit wazee kwa vijana wanawake kwa watoto, humiminika kupokea mazuwaru wa Arubaini wanaopita hapa mkoani kuelekea kwa bwana wa mashahidi (a.s), hususan wale wanaokuja kutoka kwenye mipaka ya mkoa huu”.

Akaongeza kuwa “Idadi ya mawakibu zinazoshiriki mwaka huu kuhudumia mazuwaru ni zaidi ya elfu tatu, sambamba na nyumba za wakazi waliofungua milango na kuhudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaendelea kusema “Mazuwaru wanatembea (km 260) hadi wafike Karbala kwa kutumia njia tofauti” akasema “Mkoa wa Waasit umejaa mazuwaru wanaokwenda Karbala na wahudumu wanaogawa chakula na vinyaji kwa mazuwaru”.

Mkoa wa Waasit ni kituo kikubwa cha mazuwaru wanaotoka Iran, Pakistan, India, Afghanistan na maeneo mengine ya mipaka, wanaokwenda kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: