Maukibu (4900) zimeshiriki kuhudumia mazuwaru wa Arubaini katika mkoa wa Diwaniyya.

Zaidi ya maukibu (4900) zimeshiriki kuhudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Diwaniyya, sambamba na mamia ya nyumba zilizofungua milango na kuhudumia mazuwaru.

Kiongozi anayewakilisha maukibu za mkoa huo Sayyid Ali Mahadi Radhi amesema “Idadi rasmi ya mawakibu zilizoshiriki mwaka huu katika kuhudumia mazuwaru imefika (4900), aidha kuna mawakibu ambazo hazikusajiliwa na nyumba zilizo fungua milango na kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Mkoa huu ni kituo kikubwa cha kukutana mazuwaru wa mikoa tofauti, kisha wanaelekea Hilla- Karbala, au Najafu -Karbala”.

Akabainisha kuwa “Mazuwaru wametembea umbali wa (km 511) kuanzia kituo cha kwanza cha Raasu-Bisha, wanatarajia kutembea (km129) hadi kufika mjini Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: