Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kinatumia mitambo ya kisasa kubeba mazuwaru ndani ya mji wa Karbala.
Kazi hiyo inasimamiwa na idara ya uhakiki wa mitambo ya kielektronik chini ya kitengo hicho.
Kiongozi wa idara Sayyid Ghaith Dhiyaabu Kaadhim amesema “Idara ya uhakiki inatumia mitambo ya kisasa iliyowekwa kwenye maeneo makuu yafuatayo “Mlango wa Baghdad, Hauraa, Jannatul-Hussein, Alqami, Fushah Mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Kazi ya kitengo hicho imegawanyika sehemu mbili, kwanza kuhakiki mitambo yote inayofanya kazi katika eneo la mji wa zamani na kukagua vitambulisho vya watumishi na kuwatambua kupitia uongozi mkuu wa Ataba, sehemu ya pili mitambo hiyo inasaidia kuongoza mazuwaru watukufu sehemu za hoteli zao, husseiniyya, viwanja vya kupumzika sambamba na kuwasaidia kufika sehemu wanazokusudia”.