Mawakibu za kuomboleza zimeanya matembezi mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika siku ya kumi na sita Saraf.
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Aqiil Yaasiri amesema “Mawakibu za kuomboleza za Zanjiil zimekuja kutoka mikoa tofauti ya Iraq kuhuisha matembezi ya Arubaini, kama ilivyo pangwa kuwa siku ya mwezi 16 na 17 ya mwezi huu jioni ni siku ya mawakibu za Zanjiil”.
Akaongeza kuwa “Maukibu zimeanza matembezi yao kwenye kituo kilicho karibu na malalo ya Imamu Hussein (a.s), zikapita ndani ya malalo hiyo na kisha kuelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu”
Akaongeza kuwa “Waombolezaji wamepaza sauti za kuonyesha mapenzi yao na utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s)”.
Akasisitiza kuwa “Kitengo kimeandaa watu maalum ambao wanatembea pamoja na kila maukibu kuanzia mwanzo hadi mwisho, watu hao wanajukumu la kuongoza matembezi na kuhakikisha hautokei msongamano wowote au kugongana baina maukibu moja na nyingine”.