Atabatu Abbasiyya tukufu imeratibu majlisiya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), mbele ya kiongozi wake wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na mawaidha kutoka kwa Shekhe Abdullahi Dujaili, aliye zungumza kuhusu kifo cha Imamu Hussein (a.s) na utukufu wa ziara ya Arubaini.
Aidha ameongea kuhusu msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) na kurudi kwao katika ardhi ya Karbala, sambamba na kueleza athari za safari hiyo katika kuonyesha haki.
Majlisi zinafanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya kuanzia mwezi kumi na sita Safar hadi mwezi ishirini, inahudhuruwa na wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kundi la mazuwaru.