Maukibu ya Ameed bani Hashim (a.s) chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, inatoa huduma kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara ya Arubaini.
Maukibu inatoa huduma kwa mwaka wa tano mfululizo kwa usimamizi wa kituo cha elimu na utafiti chini ya kitengo cha Habari na utamaduni.
Miongoni mwa huduma ambazo zimekuwa zikitolewa kila mwaka ni, chakula cha asubuhi kwa watu zaidi ya (1000) na kiwango kikubwa cha juisi ya baridi wakati wa mchana, kiwango huongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya mazuwaru.
Maukibu ya Ameed bani Hashim ilianzishwa mwaka (2019m) kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru wa Arubaini wanaokuja Karbala tukufu.