Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya anaangalia huduma zinazotolewa na kitengo cha mgahawa (Mudhifu) kwa mazuwaru wa Arubaini.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini ametembelea kitengo cha mgahawa (Mudhifu) na kuangalia huduma zinazotolewa kwa mazuwaru wa Arubaini .

Muheshimiwa katibu mkuu ameangalia huduma tofauti zinazotolewa na mgahawa huo kwa mamilioni ya watu wanaokuja kutoka ndani na nje ya taifa kushiriki kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Akasisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru, na kushirikiana katika kufanikisha swala hilo.

Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya umekuwa ukitoa huduma bora daima inayo endana na idadi kubwa ya watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: