Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya inafanya harakati za kidini na kitamaduni kwenye Barabara inayotumiwa na mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Kiongozi wa idara bibi Taghridi Tamimi amesema “Majengo ya Shekhe Kuleini yaliyopo Barabara ya (Baghdad – Karbala), yanashuhudia idadi kubwa ya mazuwaru wanaoshiriki kwenye harakati zake mbalimbali”.
Akaongeza kuwa “Mazuwaru wa kike hupewa zaidi ya mishumaa (1000) kwa siku, jambo hilo linafanywa kila siku kwenye eneo la bustani na Barabara za ndani ya majengo ya Shekhe Kuleini, ili kuwafanya mazuwaru wahisi utukufu wa kutembea kwao na kuwa karibu na Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Idara inategemea kufikisha ujumbe wa kidini na kitamaduni kuhusu mwenendo wa Ahlulbait (a.s) kupitia harakati tofauti inazofanya kwa mazuwaru wa Arubaini.