Majengo ya Shekhe Kuleini katika Atabatu Abbasiyya, yaliyopo Barabara ya (Baghdad – Karbala) yanatoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa Arubaini, ikiwa ni pamoja na chakula.
Kiongozi wa Majmaa Sayyid Ali Mahadi Abbasi amesema “Wahudumu wa Majmaa wanagawa maelfu ya Sahani za chakula (asubuhi, mchana na jioni), wanatoa huduma za matibabu kwa mazuwaru wanaokwenda Karbala kupitia Barabara ya (Baghdad – Karbala) kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Aidha wanagawa (juisi, matunda, vitafunwa na halwa) mbele ya majengo ya Majmaa sehemu wanayopita mazuwaru, sambamba na kugawa maji baridi ya kunywa kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha joto”.
Miongoni mwa huduma zingine zinazotolewa ni kujibu maswali kutoka kwa mazuwaru, pia kunakituo cha waliopotelewa, kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani, huduma ya choo na zinginezo.