Rais wa kitengo cha usafiri amesema “Baada ya kuwepo ongezeko kubwa la mazuwaru katika Barabara ya Najafu, Atabatu Abbasiyya imetuma gari (110) zenye ukubwa tofauti kwa ajili ya kupeba mazuwaru na kupunguza msongamano.
Akaongeza kuwa “Gari za Atabatu Abbasiyya zinabeba mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kuanzia nguzo ya (662) iliyopo katika eneo la Haidariyya kadi makao makuu ya mkoa wa Najafu”.
Akasisitiza kuwa “Watumishi wetu wanafanya kazi ya kubeba mazuwaru muda wote ili kupunguza msongamano ndani ya mji”.