Kitengo cha habari na utamaduni kinatoa huduma ya (kuhesabu watembea kwa miguu) kupitia App ya Haqibatumu-Umin.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa huduma ya kuhesabu mazuwaru wa Arubaini wanaotembea kwa miguu kwa kutumia App ya Haqibatumu-Umin.

Mkuu wa kamati ya App na program chini ya kitengo hicho amesema “Kituo kimeandaa program maalum ya kuhesabu mazuwaru wa Arubaini, na inawawezesha kutambua idadi ya hatua na masfa waliyotembea, Pamoja na umbali uliobaki kufika kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Hatua zilizosajiliwa hadi sasa zimefika (8,132,113,600), idadi ya waliotumia ni (185,100)”.

Akaendelea kusema “Kituo cha program za App ya Haqibatumu-Umin, kimeandaa program maalum ya Ziara ya Arubaini yenye ziara, dua, muongozo kwa zaairu, kuhesabu hatua na kuongoza waliopotea”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: