Muandishi wa habari katika Atabatu Husseiniyya amepongeza huduma zinazotolewa na kituo maalum cha habari za ziara ya Arubaini.

Ugeni wa kitengo cha habari katika Atabatu Husseiniyya umepongeza huduma zinazotolewa na kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kituo maalum cha habari za ziara ya Arubaini.

Rais wa kitengo Mhandisi Abbasi Khafaji amesema “Tumeangalia huduma zinazotolewa na kituo cha Habari kilichoanzishwa na Atabatu Abbasiyya, kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa habari za ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein, hakika ni kituo muhimu na kinamatokeo mazuri”.

Akaongeza kuwa “Tunapongeza jambo hili kwani limerahisisha upatikanaji wa habari kwa waandishi wa habari waliokuja kuriboti habari za ziara ya Arubaini kutoka nchi tofauti, aidha kinasaidia kufikisha ujumbe wa kifo cha Imamu Hussein (a.s) kila sehemu ya dunia”.

Ujumbe wa mazuwaru umetembelea sehemu mbalimbali za kituo maalum cha habari katika Atabatu Abbasiyya na kuangalia huduma zinazotolewa katika siku za ziara hii tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: