Mkuu wa ofisi ya muwakilishi wa Sayyid Sistani nchini Iran amepongeza huduma zinazotolewa na majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Shekhe Kadhim Muhammad Taqi Aljawahiri Mkuu wa ofisi ya Sayyid Jawadi Shahristani, Muwakilishi Mkuu wa Sayyid Ali Sistani nchini Iran, amepongeza huduma zinazotolewa na majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mazuwaru wa Arubaini.


Wamepokewa na msimamizi Mkuu wa Majmaa na mjumbe wa kamati ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Jawad Hassanawi katika majengo hayo yaliyopo Barabara ya  (Njafu - Karbala).


Ziara hiyo ni sehemu ya kuangalia huduma mbalimbali zinazotolewa na majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).


Majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yanatoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa Arubaini, ikiwa ni pamoja na ugawaji wa chakula,malazi na huduma za afya.

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: