Sayyid Swafi amekutana na ujumbe wa taasisi ya afya ya kimataifa Al-Imamiyya.

kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amekutana na wajumbe wa Taasisi ya Afya ya kimataifa Al-Imamiyya.


Kiongozi wa shughuli za udaktari katika Atabatu Abbasiyya Haifa Tamimi amesema "Ujumbe unajumuisha madaktari na wauguzi wa fani tofauti,Waliokuja Karbala kushiriki kuhudumia mazuwaru wa Arubaini".


Akaongeza kuwa "Wageni hao wamefafanua kuhusu kazi zao na huduma wanazotoa, Muheshimiwa Sayyid amepongeza kazi nzuri wanayofanya ya kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s), wakaongea kuhusu uwezekano wa kutoa mafunzo ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza kwa watumishi wa Ataba.


Mjumbe wa Taasisi hiyo kutoka nchi ya Hangari amesema "Nashukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutupa nafasi ya kushiriki kutoa huduma na kutoa mafunzo ya uokozi kwa watumishi waliopo kwenye vituo vya afya".


 


 

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: