kundi kubwa la mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq linahusisha usiku wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi.
mji wa Karbala umepokea mamilioni ya watu waliokuja kutoka kila sehemu ya Dunia kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), huku wakiwa wamejaa huzuni na majonzi kutokana na msiba huo mkubwa kwa Ahlulbait (a.s).
atabatu Abbasiyya inafanya kila iwezalo kutoa huduma bora kwa mazuwaru chini ya mkakati maalum, ikiwa ni pamoja na kugawa chakula, maji na mambo mengine.
mawakibu zinaendelea kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru na kufanya majlisi za kuomboleza pamoja na mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).