Atabatu Abbasiyya imetangaza idadi ya mazuwaru walioshiriki kuhuisha ziara ya Arubaini.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, leo siku ya Jumatano (20 Safar 1445h) sawa na (6 Septemba 2023m), umetangaza idadi ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), iliyopatikana kupitia mitambo ya kuhesabu watu wanaoingia katika mji mtukufu wa Karbala.

Lifuatalo ni tamko rasmi kutoka kwenye uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya:

Tunatoa rambirambi kwa Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.s) na maraajii watukufu na ulimwengu wa kiislamu, hususan Iraq taifa la Mitume, Mawasii na Mawalii kwa kumbukizi ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu alinde miji ya waislamu kutokana na kila aina ya ubaya, na awarudishe mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein katika nchi zao na miji yao wakiwa salama na wenye kukubaliwa ibada zao.

Kama kawaidha yetu kwa zaidi ya karne (13), mji wa Karbala umepokea mazuwaru wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika msimu wa ziara tukufu ya Arubaini ya mwaka 1445h, wahudumu wa Ataba wamepata utukufu mkubwa kwa kupokea na kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru hao, miongoni mwa huduma hizo ni kuhesabu mazuwaru kwa kutumia mitambo ya kisasa iliyofungwa kwenye Barabara kuu za kuingia Karbala chini ya usimamizi wa idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya kwa mwaka wa nane mfululizo.

Idadi ya mazuwaru walioingia katika mji mtukufu wa Karbala kuanzia tarehe 1 Safar hadi tarehe 20 Safar saa 6:00 Adhuhuri kwa mujibu wa mitambo ya kuhesabu watu iliyofungwa kwenye Barabara kuu nne za (Bagdad – Karbala, Najafu – Karbala, Baabil – Karbala, Husseiniyya – Karbala) imefika (22,019,146), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akubali ibada zao na atuwafikishe kufanya mambo anayoyapenda na kuyaridhia hakika yeye ni mwingi wa kusikia na kujibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: