Majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ya kuhudumia mazuwaru yamehitimisha kazi zake kwa kufanya Majlisi ya kuomboleza.

Majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ya kuhudumia mazuwaru chini ya Atabatu Abbasiyya, yamehitimisha kazi zake kwa kufanya Majlisi ya kuomboleza.

Majlisi imehudhuriwa na msimamizi kuu wa majengo hayo na mjumbe wa kamati kuu katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Jawadi Hasanawi, rais wa kitengo cha sheria Sayyid Muhammad Fatalawi, makamo rais wa kitengo cha Dini Shekhe Aadil Wakiil, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) waliotoa huduma kwenye majengo hayo katika siku za ziara ya Arubaini, pamoja na wahudumu wa kujitolea.

Majengo hayo yapo Barabara ya (Najafu – Karbala) yamehitimisha huduma zake leo, baada ya kuisha misafara ya mazuwaru kwenye Barabara hiyo, sambamba na kuhitimisha shughuli za wahudumu wa kujitolea kutoka taasisi ya Qamaru Bani Hashim kwa mazuwaru wa Arubaini kwenye majengo hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: