Kitengo cha usafiri katika Atabatu Abbasiyya kimetumia zaidi ya gari (300) kubeba mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Rais wa kitengo hicho Mhandisi Alaa Jaburi amesema “Tumetumia basi (308) pamoja na gari zingine ndogo kubeba mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kuwapeleka nje ya mji wa Karbala kwa lengo la kupunguza msongamano uliopo ndani ya mji huu kwa sasa”.
Akaongeza kuwa “Hatua ya kwanza ilianza siku ya kwanza ya mwezi wa Safar, kwa kubeba mazuwaru kutoka kwenye vituo vya nje ya mji na kuwaleta ndani ya mji wa Karbala, hatua ya pili tunawatoa ndani ya mji na kuwapeleka kwenye vituo vya nje ya mji wa Karbala, ambako wanaanzia safari zao za kwenda mikoani kwao”.
Akasema kuwa: “Baada ya kukamilika kwa kazi nzuri ya kuhudumia mazuwaru, wahudumu wa kujitolea wanabebwa na gari zetu na kuwarudisha mikoani kwao”.
Akabainisha kuwa “Gari za kufanya usafi bado zinaendelea na kazi”.