Baada ya kumaliza ziara ya Arubaini.. maukibu ya (Binafsi Anta) inaendelea kuhudumia mazuwaru katika mji wa Karbala.

Maukibu ya Binafsi Anta inayosimamiwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea kuhudumia mazuwaru pamoja na kumalizika kwa msimu wa ziara ya Arubaini.

Kiongozi wa idara ya ufatiliaji katika idara ya habari chini ya kitengo hicho Sayyid Alaa Hamdi Matwaru amesema “Maukibu ilianza kutoa huduma tangu mwezi kumi Safar katika mji wa zamani eneo ya –Baabu Khaani- nab ado inaendelea kutoa huduma baada ya kuisha kwa ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa “Tutaendelea kuhudumia mazuwaru watukufu hadi mwezi 23 Safar, kwani bado kunaidadi kubwa ya mazuwaru katika mji mtukufu wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: