Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha maandalizi ya kuhifadhisha Qur’ani tukufu baada ya likizo ya ziara ya Arubaini.
Maandalizi yamehusisha matengenezo ya vipaza sauti, kumbi za masomo, kumbi za michezo ya kiakili na kumuili sambamba na kuandaa ukumbi maalum kwa ajili ya maelekezo ya kinafsi na kimalezi, kwa ajili ya kuanza masomo ya kuhifadhisha Qur’ani tukufu.
Maandalizi hayo yanalenga kuweka mazingira mazuri ya kuhifadhi Qur’ani tukufu katika Maahadi ya Qur’ani.