Msimamizi wa usafi Sayyid Amiri Mussawi amesema “Baada ya kumaliza ibada ya ziara na kupokea mamilioni ya watu, watumishi wetu wameanza kazi kusafisha uwanja huo na kubadilisha mazulia”.
Akaongeza kuwa “Kazi kubwa ya usafi hufanywa kila baada ya ziara inayohudhuriwa na mamilioni ya watu na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za kidini na kitamaduni”.
Kitengo kimetoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) waliokuja kuhuisha ziara ya Arubaini toka siku ya kwanza ya mwezi wa Safar.