Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeanza kutoa masomo ya tahfiidh na hukumu za tajwidi baada ya likizo ya ziara ya Arubaini katika mji wa Najafu.
Kiongozi wa idara ya harakati katika Maahadi ya Qur’ani mjini Najafu Sayyid Zaidi Maduhi Rimahi amesema “Wanafunzi wa Maahadi wameanza kusoma Qur’ani na kufuatilia masomo yao ya kila siku kwa mujibu wa ratiba”.
Akaongeza kuwa “Pamoja na ratiba za masomo ya darasani, kuna ratiba ya safari za kidini ndani na nje ya taifa”.
Kuna jumla ya wanafunzi (125) katika makundi saba ya viwango tofauti vya kuhifadhi, huku wanafunzi (12) wakimaliza kuhifandhi kitabu chote cha Mwenyezi Mungu mtukufu.