Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimechapicha kitabu cha (Katalogi ya kaburi za pamoja nchini Iraq – wakati wa chama cha Baathi).
Mkuu wa kituo cha kuthibitisha jinai za magaidi Dokta Abbasi Quraishi amesema “Toleo jipya linaonyesha utendaji wa kituo katika kuthibitisha jinai za magaidi”.
Akabainisha kuwa “Kitabu hiki kinaonyesha kaburi za pamoja na jinai zilizofanywa na chama cha Baathi nchini Iraq”.
Akaongeza kuwa “Kitabu kimeandika kwa ufupi kuhusu kaburi za pamoja nchini Iraq na mauwaji ya kutisha yaliyofanywa na chama cha Baathi, kituo kinalenga kuwajulisha raia wa Iraq mateso waliyopitia wakati wa utawala wa chama cha Baathi kilicho ondolewa madarakani”.