Atabatu Abbasiyya imewekwa mapambo meusi na mabango yanayoashiria huzuni ya kumbikizi ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Makamo rais wa kitengo cha usimamizi wa haram Shekhe Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Tumeanza kuweka mapambo yanayoashiria huzuni kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), katika haram tukufu na milango ya Ataba takatifu baada ya kuondoa mapambo yanayohusu ziara ya Arubaini”.
Akaongeza kuwa “Mabango yamewekwa ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tumetumia vifaa maalum katika uwekaji ili iwe rahisi wakati wa utoaji wa mapambo hayo”.
Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huo kwa kufanya Majlisi na kutoa mawaidha, sambamba na kukumbusha nafasi ya Mtume wetu mtukufu (s.a.w.w) katika kutangaza ujumbe wa kiislamu.