Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, kiligawa zaidi ya barafu elfu (40) wakati wa ziara ya Arubaini.
Makamo rais wa kitengo Mhandisi Abbasi Ali amesema “Wahudumu wa kitengo walianza kugawa maji safi ya kunywa na barafu toka siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam, walisambaza deli (350) za kutunzia maji na barada (24) katika maeneo yanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na Barabara zinazo zunguka sehemu hiyo”.
Akaongeza kuwa “Watumishi wa kikitengo chetu wanagawa barafu (2000) zenye uzito wa kilo (35) kila moja kwa mawakibu zilizopo katika mji wa Karbala wakati wote wa mwezi wa Safar”.
Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo amesema “Kiwanda cha barafu kilikuwa kinatengeneza barafu elfu (40) wakati wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kuzigawa kwa mawakibu Husseiniyya zilizokuwa zinahudumia mazuwaru wa Arubaini”.