Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imepanga muda wa kufanya jaribio kwa wanafunzi walio omba nafasi za masomo kwenye maahadi yake.

Maahadi ya wahadhri wa Husseiniyya chini ya idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza muda wa jaribio kwa wanafunzi walio omba nafasi za masomo kwenye Maahadi yake.

Maahadi imesema kuwa siku ya Jumapili ya kwanza katika mwezi wa Rabiul-Awwal mwaka 1445h sawa na (17/9/2023m) saa tatu asubuhu kutakuwa na jaribio la wanafunzi wapya kwenye kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) katika mji wa Karbala.

Kwa wote waliotuma maombi ya masomo wafike sehemu tajwa kwa muda uliotajwa, kumbuka kuwa mlango wa usajili bado uko wazi kwa kila anayetaka kujiunga na masomo na mwenye sifa.

Maahadi ipo mtaa wa Mulhaqu/ Barabara ya hospitali ya Husseini (a.s) karibu na chuo cha Swahibu Zamaan (a.f) kwenye kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) ghorofa la kwanza/ idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: